Skip to content Skip to footer

Chumbe Island is a launching partner of the Zanzibar Sustainable Tourism Declaration

Kisiwa cha Chumbe ni mshirika wa uzinduzi wa Azimio la Zanzibar la Utalii Endelevu, lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar

The Declaration paves the way for tourism stakeholders from Zanzibar to take action and actively collaborate for a tourism that benefits the people and natural and cultural heritage of Zanzibar.

Azimio hilo linafungua njia kwa wadau wa utalii kutoka Zanzibar kuchukua hatua na kushirikiana kikamilifu kwa ajili ya utalii wenye manufaa kwa wananchi na urithi wa asili na utamaduni wa Zanzibar.

Chumbe Island participated at the Zanzibar Tourism Investment and Travel Exhibition (ZTITE) under the theme of ‘Greener Zanzibar’ and assisted the official launch of the Zanzibar Sustainable Tourism Declaration, which was attended by high level dignitaries and accompanied by a panel discussion on sustainable tourism in Zanzibar.

Kisiwa cha Chumbe kilishiriki katika Maonesho ya Uwekezaji na Utalii Zanzibar (ZTITE) chini ya kaulimbiu ya ‘Zanzibar ya Kijani’ na kusaidia uzinduzi rasmi wa Azimio la Zanzibar la Utalii Endelevu, uliohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu na kuambatana na mjadala wa majadiliano uliozungumzia Utalii Endelevu Zanzibar.

As part of our vision to effectively manage and protect Chumbe Island, we strive to serve as a model for effective ecotourism and MPA management and provide a platform to promote wider environmental awareness for sustainable development and ecological stewardship in Zanzibar. In line with our efforts to promote sustainable tourism development in the destination Zanzibar, we have been contributing to a Working Group spearheaded by the Ministry of Tourism and Heritage through the Zanzibar Commission for Tourism to find suitable approaches to foster public-private partnerships and action for sustainable development of tourism in the Blue Economy.

Kama sehemu ya dira yetu ya kusimamia na kukilinda Kisiwa cha Chumbe, tunajitahidi kuwa kielelezo cha ufanisi wa utalii wa ikolojia na usimamizi wa MPA na kutoa jukwaa la kukuza uelewa mpana wa mazingira kwa maendeleo endelevu na utunzaji wa ikolojia Zanzibar. Sambamba na juhudi zetu za kukuza maendeleo endelevu ya utalii Zanzibar, tumekuwa tukichangia katika Kikundi Kazi kinachoongozwa na Wizara ya Utalii na Maliasili kupitia Kamisheni ya Utalii Zanzibar kutafuta mbinu mwafaka za kukuza mashirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na kuchukua hatua kwa maendeleo endelevu ya utalii katika Uchumi wa Bluu

Chumbe Island is proud to have helped to develop the Zanzibar Sustainable Tourism Declaration, which was launched and officially endorsed on Thursday February 9th 2023 at the ZTITE at the Peace Memorial by the President of the Revolutionary Government of Zanzibar, H.E. Dr Hussein A. Mwinyi in attendance of high level representatives from public and private sector. The championing of the declaration and the event by His Excellency signals sustainability is supported at the highest levels in Zanzibar.

Kisiwa cha Chumbe kinajivunia kusaidia kuanzisha Azimio la Zanzibar la Utalii Endelevu, ambalo lilizinduliwa na kutiwa saini rasmi Alhamisi Februari 9, 2023 katika ukumbi wa ZTITE Peace Memorial na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Dk Hussein A. Mwinyi katika mahudhurio ya wawakilishi wa ngazi za juu kutoka sekta ya umma na binafsi. Ushindi wa tamko hilo na tukio hilo la Mheshimiwa kunaashiria uendelevu unaungwa mkono katika ngazi za juu kabisa za Zanzibar.

In a panel discussion consisting of Dr Mwatima Juma (Msonge Farm/Permaculture Institute of Zanzibar), Ben Taylor (Manager of CHICOP), Robert Wild (Space for Nature/York University), Dr. Makame Omar Makame (Ministry of Blue Economy and Fisheries) and Mr. Sheha Mjaja (Zanzibar Environmental Management Authority) moderated by Diana Körner, panelists discussed the challenges and changes ahead in making the Zanzibar tourism industry more sustainable.

Katika mjadala uliojumuisha Dk Mwatima Juma (Shamba la Msonge/Taasisi ya Permaculture Zanzibar), Ben Taylor (Meneja wa CHICOP), Robert Wild (Space for Nature/York University), Zahor El Kharousy (Wizara ya Uchumi wa Buluu) na Farhat Nassor, (Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar) ikisimamiwa na Diana Körner, wanajopo walijadili changamoto na mabadiliko yatakayotokea katika kuifanya sekta ya utalii Zanzibar kuwa endelevu zaidi.

The Zanzibar Sustainable Tourism Declaration sets out to support this journey, as it is an informal statement of intent and a rallying cry for the Zanzibar tourism industry to take real strides towards sustainability, in support of people, planet and prosperity. It recognizes the effects that tourism is having on the natural and cultural environment of Zanzibar and the collective responsibility that each segment of society has in the process of ensuring that tourism brings the desired cultural, economic, and environmental benefits.

Specifically, the Declaration sets out five areas of commitment for its first year, namely ‘Sustainable food from land and sea’, ‘Sustainable waste management’, ‘Space for Nature and restoring ecosystems’, ‘Support local Zanzibar culture, knowledge and expertise’, and ‘Reduce greenhouse gas emissions in our operations’, which give signatories a direction of action for making their tourism operations more sustainable.

Signatories can choose three of the five commitments they wish to focus on and thereby pledge to work on proposed areas of improvement and possible tangible targets. The Declaration is all about education and collaboration. Each area of commitment will set up its own Working Group with members from public and private sector, academia and NGO. The overall Declaration is aligned with international processes and initiatives such as the UNWTO Glasgow Declaration on Climate Action and encourages Zanzibari signatories to be part of a wider global movement to create a more prosperous industry and destinations for our future generations and our planet.

Azimio la Zanzibar kuhusu Utalii Endelevu linakusudia kuunga mkono safari hii, kwani ni kauli isiyo rasmi ya dhamira na kilio cha hadhara kwa sekta ya utalii ya Zanzibar kupiga hatua za kweli kuelekea uendelevu, katika kuunga mkono watu, sayari na ustawi. Inatambua athari zinazotokana na utalii katika mazingira asilia na kitamaduni ya Zanzibar na wajibu wa pamoja ambao kila sehemu ya jamii inao katika mchakato wa kuhakikisha kwamba utalii unaleta manufaa yanayotarajiwa ya kiutamaduni, kiuchumi na kimazingira.

Hasa, Azimio linaweka maeneo matano kama ni kipaumbele kwa mwaka wake wa kwanza, ambayo ni ‘Chakula Endelevu kutoka nchi kavu na baharini’, ‘Udhibiti endelevu wa takataka’, ‘Nafasi kwa ajili ya Asili na kurejesha mifumo ikolojia’, ‘Kusaidia utamaduni wa Zanzibar, maarifa na utaalamu’, na ‘Kupunguza uzalishaji wa gesi chafu katika shughuli zetu’, ambayo huwapa watia saini mwelekeo wa hatua ya kufanya shughuli zao za utalii kuwa endelevu zaidi.

Watia saini wanaweza kuchagua vipaumbele vitatu kati ya vitano wanavovitaka kuvizingatia na hivyo kuahidi kufanyia kazi maeneo yaliyopendekezwa ya uboreshaji na shabaha zinazoonesha zinawezekana. Azimio linahusu elimu na ushirikiano. Kila eneo la kujitolea litaanzisha kikundi chake cha kufanya kazi na wanachama kutoka sekta ya umma na ya kibinafsi, wasomi na taasisi zisizo za kiserikali. Azimio la jumla linawiana na michakato na mipango ya kimataifa kama vile Azimio la UNWTO Glasgow juu ya Hatua ya hali ya hewa na inawahimiza wazanzibari waliotia saini kuwa sehemu ya harakati pana zaidi za kimataifa ili kuunda tasnia yenye ustawi zaidi na mafikio kwa vizazi vyetu vijavyo na sayari yetu.

Go to Top