The Chumbe Island team is excited to launch a series of ‘Green Destination’ workshops taking place on the island in the coming weeks. There will be four workshop themes: sustainable waste management, marine conservation, sustainable seafood as well as island biodiversity and natural history. In total there are eight possible workshop dates to accommodate as many tourism stakeholders as possible.
Timu ya Kisiwa cha Chumbe inafuraha kufanya warsha ya ’ Green Destination’ itakalofanyika kisiwani Chumbe wiki zijazo. Warsha hii itakuwa na mada (theme) nne: Usimamizi endelevu wa takataka, Uhifadhi wa bahari, Uendelevu wa chakula bahari na vile vile Bioanuai ya kisiwa na historia ya asili
The first workshop today (02nd September) focused on sustainable waste management. The Chumbe team presented solutions for reducing, reusing and recycling waste in tourism operations and discussions focused on how we can achieve a circular economy of waste. Guest speakers from Chumbe’s partner organisations Ozti, Chako, Zanrec, the Practical Permaculture Institute of Zanzibar and Chanzi shared information on their recycling initiatives. Participants received a tour of Chumbe’s eco architecture and learned about Chumbe’s ‘zero-impact’ waste management systems, including the elimination of single-use plastics, composting toilets and vegetative grey water filtration systems.
Warsha ya kwanza ni leo (02/Septemba) itahusu usimamizi endelevu wa takataka. Timu ya Chumbe itaongelea suluhisho katika dhana ya Kupunguza, Kutumia tena, Kurejesha takataka katika shughuli za utalii na mazungumzo yatalenga ni namna gani tunaweza kufikia mduara wa uchumi kwa kutumia takataka. Wageni wasemaji kutoka wadau wa Chumbe ni kutoka Ozti, Chako, zanrec, Taasisi ya ufugaji wa swamaki ya Zanzibar na Chanzi hawa watatoa maelezo kuhusiana na recycling. Washiriki watatembelea nyumba za kimazingira za Chumbe na kujifunza vipi Chumbe inafikia Zero Impact katika uangalizi wa takataka.
Participants came from a range of different institutions, such as hotels, operators, community groups, training centers and NGOs. There was a strong desire to learn from Chumbe’s green practices, and to find solutions together for sustainable business management, protection of the natural heritage and future of the Zanzibar archipelago.
Washiriki wa Warsha hii wanatoka taasisi tofauti, kama hoteli, tour operator, wanajamii, taasisi za mafunzo na NGOs. Kumekua na hamu kubwa ya watu kutaka kujifunza kupitia Uzoefu uliopo Chumbe kuhusu Green practices na kutafuta suluhisho la pamoja kwa ajili ya kuwa na uangalizi wa biashara endelevu,hifadhi ya urithi asilia na hatma ya kisiwa cha Zaznzibar.
The workshops are part of a wider ‘Green Destination’ campaign, supported by the German Ministry for Development Cooperation (BMZ). Participation is free of charge for tourism professionals from Zanzibar and all transport and lunch is provided. Registration is required however, (and places are filling fast!). For more information, and to register for participation, contact marketing@chumbeisland.com
Kongamano hili ni sehemu ya kampeni kubwa ya Green Destination (Eneo la Kijani) inayodhaminiwa na Wizara ya maendele na ushirikiano ya Ujerumani (BMZ). Hakutakuwa na gharama ya kushiriki kwenye warsha hii , Usafiri na chakula vitakuwepo. Hata hivyo kujiorodhesha kunahitajika, (na nafasi zinajazwa haraka). Kwa maelezo zaidi, kwa usajili wa washiriki wasiliana na marketing@chumbeisland.com