Chumbe Island celebrates community swimming program participants and environmental champions – Kisiwa cha Chumbe kusherekea Kumalizika kwa mafunzo ya kuogelea Na washindi wa mazingira

In an official certification ceremony at the Old Fort in Stone Town on Saturday January 22nd 2022, Chumbe Island Coral Park and its swimming partners Panje and FitPit celebrated the 300 participants of their community swimming program as well as community members who contributed to a series of environmental competitions.

Katika sherehe maalum ya kuwatunuku vyeti katika ukumbi wa Ngome Kongwe mji Mkongwe siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022, Kisiwa cha Chumbe na washirika wake wa kutoa mafunzo ya kuogelea Panje na FitPit walisherehekea kufuzu kwa washiriki 300 katika mpango wao wa mafunzo kwa jamii ya kuogelea pamoja na wanajamii wengine ambao walishiriki katika mashindano mbali mbali ya mazingira.

“Karibu Zanzibar” the song produced in partnership with Stone Town Records, sung by the three winners of Chumbe Island’s community song competition was one of many highlights performed live on stage on Saturday at the official certification ceremony of a number of community activities Chumbe Island has conducted over the past couple of months in close partnership with Panje and financed by the German Ministry of Development Cooperation (BMZ) under developpp.

“Karibu Zanzibar” ni wimbo uliotungwa na kurekodiwa kwa mashirikiano ya Stone Town Records na ulioimbwa na Washindi watatu wa mwanzo wa shindando la nyimbo lililoandaliwa na Kisiwa cha Chumbe, wimbo huo ulikuwa ni moja kati ya yaliyokuwepo na uliimbwa mubashara kwenye jukwaa siku ya Jumamosi katika sherehe za kukabidhi vyeti kwa washiriki wa shughuli mbalimbali ambazo Kisiwa cha Chumbe ilizifanya kwa ushirikiano wake wa Karibu na Panje ambapo shughuli hizi zilifadhiliwa na Shirika la Ujerumani la Maendeleo na Mashirikiano (BMZ) chini ya Mradi wa developpp.

As part of a project supported by BMZ, Chumbe Island developed the “Safety at Sea” Swimming Program for local community members of different ages. The program took place over the period from September/October 2020 to January 2022 and developed a detailed training methodology in partnership with the local NGO Panje. A train-the-trainer approach was rolled out for a total of 22 community members, which were certified as swimming coaches (including 1 employee from Chumbe Island) and a total of 300 community members learned how to swim in this period. Target groups for the swimming program were non-swimming CHICOP employees, education establishment personnel (school teachers and educationalists), as well as marine-related practitioners (fishers, seaweed and sponge farmers, boat crews, tour guides, KAWA NGO youth training center, etc.). The participants proudly collected their certificates on the stage of the Old Fort and were handed a copy of the Kiswahili “Usalama Baharini” safety at sea handbook.

Ikiwa ni sehemu ya Mradi uliodhaminiwa na BMZ, Kisiwa cha Chumbekilianzisha mafunzo ya kuogelea ya “ Uslama Baharini” kwa ajili ya wanajamii wa umri tofauti. Mafunzo haya yalianzi katika mwezi wa Septemba/Oktoba 2020 mpaka Januari 2022 na kuliratibiwa njia bora za ufundishaji kwa mashirikiano na NGO ya Panje.Mwanzo kulitafutwa na kulifundishwa zaidi wakufunzi wa mafunzo hayo wapatao 22 kutoka miongoni mwa jamii, ambao walikuwa ni walimu wa mafunzo hayo (Mmoja wao alikuwa ni muajiriwa wa Chumbe) Na katika kipindi hichi jumla ya wanajamii 300 walijifunza kuogelea. Makundi lengwa katika mafunzo haya ya kuogelea ni wafnyakazi wa Chumbe wasiojua kuogelea, walimu wa maskuli na wanataaluma wengine pamoja na watu wanaojishughulisha kazi zao na Bahari(wavuvi,wakulima wa mwani na spanji mabahria wa boti watembeza watalii na NGO ya mafunzo kwa vijana y KAWA.) Washiriki walifurahi kwa kupokea vyeti vyao katika jukwaa la Ngome Kongwe na walikabidhiwa kitabu cha Kiswahili cha “Usalama Baharini” Safety at sea handbook.

As part of the project, Chumbe Island also organized a series of community competitions and activities, for which certificates were also handed out, namely:

  • Trash-to-art village education sculpture campaign for six communities in Unguja (Dimani, Kombeni, Kiembesemaki, Nyamanzi, Buyu, Chuwani), involving beach cleanups for community members and the design of creative sculptures made from trash by the waste ambassadors to raise awareness on the challenges that waste is causing for the communities.
  • Sustainable seafood campaign, whereby Chumbe Island updated its sustainable seafood guide and incorporated stories from fishers on “fishing stories and traditions”
  • A song competition on the natural history and beauty of Zanzibar archipelago was organized which selected three community members as winners, who recorded the song “Karibu Zanzibar” in partnership with Stone Town Records and the Dhow Countries Music Academy.
  • An art competition campaign on “Marine Species Conservation” which invited community members from the six communities to submit drawings on six endangered species in Zanzibar, namely turtle, dolphin, shark, grouper, lobster and sea cucumber.

Ikiwa ni sehemu ya Mradi,Kisiwa cha Chumbe pia kilifanya mashindano mbali mbali ya wanajamii kivitendo na vyeti vile vile vilitolewa kama vile:

  • Taka-kuwa Sanaa ya kampeni ya elimu kwa vijiji sita hapa Unguja(Dimani, Kombeni,Kiembe Samaki, Nyamanzi, Buyu, Chukwani),yakihusiana na kusafisha fukwe kwa wanajamii na ubunifu wa maumbo yanayotokana na takataka hizo yaliyotengenezwa na mabalozi wa usafi ili kuweza kutoa muamko na hamasa juu ya madhara ya takatakakwa mazingira na jamii yetu.
  • Kampeni chakula endelevu cha Baharini, ambapo Chumbe iliuboresha muongozo wake wa chakula endelevu cha Baharini kwa kuongeza” hadithi na mila” kutoka kwa wavuvi.
  • Mashindano ya nyimbo juu ya historia ya maumbile na uzuri wa Kisiwa cha Zanzibar yalifanyika ambapo Washindi bora watatu kutoka kwa wanajamii walichaguliwa ambao walirikodi wimbo wa “Karibu Zanzibar” kwa mashirikiano na kituo ga kurikodia cha Stone town pamoja na Dhow countries Music Academy.
  • Mashindano ya Sanaa ya uchoraji kwa” Hifadhi ya viumbe vya Baharini” ambayo washiriki wake walitoka kutoka vijiji sita,na waliwasilisha michoro aina sita ya viumbe vya Baharini ambavyo viko hatarini kutoweka katika Zanzibar ambavyo ni kasa, pomboo, chewa,kamba kochi na jongoo bahari.

All winners of the competitions visited Chumbe Island as part of an environmental education trip. As the closing ceremony the Chumbe team thanked its partners and funders and highlighted the importance of this project to empower community members and increase their life skills and employability in the challenging times of the pandemic, as well as to raise awareness of the importance of protecting the environment through art.

Washindi wote wa mashindano hayo walipata fursa ya kutembelea Chumbe kama ni sehemu ya safari za elimu ya mazingira. Kwa kufunga sherehe hizi timu ya Chumbe iliwashukuru washirika na wafadhili na walionyesha umuhimu wa Mradi huu kwa kuwawezesha wanajamii na kwa kuongezea ujasirimali katika Maisha pamoja na kuweza kuajirika panopotokea mabalaa pamoja na kuongeza muamko juu ya kuhifadhi mazingira kwa kutumia Sanaa.